Mastaa

Alia Bhatt ageuka mwanamuziki kwenye harusi ya rafiki yake

UHISPANIA : MUIGIZAJI Alia Bhatt amevuta hisia za mashabiki wake wengi na kuwashangaza baada ya kugundua kuwa muigizaji huyo anakipaji kingine cha uimbaji baada ya kukionyesha katika sherehe ya rafiki yake nchini Uhispania.

Alia alionesha kipaji hicho cha kuimba baada ya kuwasili katika sherehe za rafiki yake Tanya Saha Gupta na mumewe David Angelov akitokea moja kwa moja nchini Ufaransa kwenye tamasha la filamu la Cannes la 2025.

Alia baada ya kufika katika ukumbi wa sherehe hiyo alijumuika katika steji na kuanza kuimba na kucheza midundo ya dhol wimbo wa Kangana Ranaut London Thumakda.
Alia Bhatt alianza kuonesha makeke yake kwenye Tamasha la Filamu la Cannes, Alivaa saree maalum na Gucci. Baadaye, alihudhuria harusi ya rafiki yake Tanya Saha Gupta huko Uhispania. Alia ataigiza katika filamu mpya ya ‘Alpha’, akitarajiwa kucheza nafasi ya Kijasusi.

Related Articles

Back to top button