Nyumbani

Simba :Hii tunabeba inahamia ndani

DAR ES SALAAM:UONGOZI wa Klabu ya Simba umeweka bayana dhamira yao ya kuhakikisha wanabeba mataji yote ya ndani msimu huu, huku wakitumia kauli mbiu yao maarufu “Hii Tunabeba” kama chachu ya mafanikio.

Simba SC imejipanga vilivyo kuhakikisha inanyakua Ligi Kuu ya Tanzania Bara pamoja na Kombe la Shirikisho la CRDB. Tayari kikosi hicho kimeondoka asubuhi ya leo kuelekea mkoani Manyara, ambako kitashuka dimbani kwenye nusu fainali ya pili dhidi ya Singida Black Stars siku ya Jumamosi, Mei 31, kwenye Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesisitiza kuwa malengo yao ni makubwa na hayana njia ya mkato ni  lazima wayafikie kwa ushindi.

“Malengo yetu ni ubingwa wa Shirikisho. Kufikia huko, hatuna budi kuwatoa Singida Black Stars. Tunajua hautakuwa mchezo rahisi kutokana na ubora wa wapinzani wetu, lakini tumejipanga vya kutosha,” ameongeza.

Ahmed ameongeza kuwa kikosi hicho kimewasili salama Babati na jioni hii kitaanza mazoezi rasmi kwa maandalizi ya mechi hiyo muhimu. Aidha, amesema mazoezi yataendelea Ijumaa, Mei 30, kwa ajili ya kuweka mikakati madhubuti ya kuwashinda wapinzani wao na kutinga hatua ya fainali.

Related Articles

Back to top button