Nyumbani

Maguli: Tumejipanga, hatutaki kurudia makosa

GEITA:MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, Elias Maguli, amesema kikosi chao kimejiandaa vilivyo kwa mchezo wa marudiano wa mtoano dhidi ya Stand United, ambao ni wa mwisho kwao na wenye umuhimu mkubwa kama fainali.

Mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita ililazimishwa sare ya mabao 2-2. Sasa watarudiana kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga Leo.

Akizungumza kuelekea mchezo huo muhimu, Maguli amesema wachezaji wa Geita Gold wamejifunza kutokana na makosa ya mchezo uliopita na sasa wanakwenda ugenini kwa mtazamo mpya na ari ya ushindi.

“Sisi kama wachezaji tumejipanga vizuri kwa ajili ya mchezo huu kwa sababu hauna marudiano tena, ni mchezo wa mwisho, ni kama fainali. Tunaangalia tulikotoka; tulikuwa nyumbani lakini tukashindwa kupata pointi tatu, jambo ambalo halikutarajiwa,” amesema Maguli.

Ameeleza kuwa licha ya kupoteza mchezo huo wa awali, kikosi chao kimechambua mapungufu yote yaliyojitokeza na kufanya maandalizi ya kurekebisha kila kilichowagharimu.

“Tunatambua mchezo huu utakuwa mgumu na ushindani mkubwa. Uwanja huu si wa timu yoyote kujihakikishia ushindi sio Stand wala Geita hawana uhakika. Lakini sisi tunaamini kuwa tukicheza kwa haki na kwa nidhamu ya mchezo, tunaweza kupata matokeo mazuri,” amesema.

Mshindi wa jumla katika mchezo huu atakutana na atakayeshindwa kwa mchezo wa mtoano kwa mechi za Ligi Kuu kati ya atakayemaliza nafasi na 13 na 14.

 

Related Articles

Back to top button