Mastaa

Thee Pluto aweka wazi alivyoachana na mama mtoto wake

NAIROBI: MUANDAAJI wa vipindi vya mtandaoni kutoka Kenya Thee Pluto ameweka wazi namna alivyoachana na mama mtoto wake Felicity Shiru.

Pluto amesema namna alivyoshindwa kuendelea na mpenzi wake akidai kwamba kwa sasa atakuwa makini atakapoanzisha uhusiano na mwanamke mwingine ili uhusiano wao usiyumbe kama wa awali.

Kulingana na Thee Pluto, anakubaliana na baadhi ya mashabiki kuwa huenda likawa ni ‘tatizo la kifamilia’ akikumbuka kwamba kaka yake Sam Tollad pia aliachana na mama watoto wake.

Zaidi ya hayo, uhusiano wa kaka yake mkubwa Dela haujakuwa tofauti na yeye hali ambayo imeibuliwa na mashabiki wake kwamba hawajui namna ya kuandaa uhusiano na kudumu nao katika baya na zuri.

Uhusiano kati ya Pluto na Felicity ulimalizika rasmi mnamo 2024, baada ya takriban miaka mitatu wakiwa pamoja. Ingawa wote wawili wameshughulikia utengano huo hadharani, sababu kamili zimesalia kuwa na utata na siri kati yao, huku pande zote mbili zikidokeza changamoto zinazohusiana na mawasiliano na uaminifu.

Mgawanyiko huo ulionekana hadharani wakati Thee Pluto alipotangaza kwenye mitandao ya kijamii kwamba Felicity alikuwa ameondoka katika makazi yao ya pamoja. Wote wawili wametoa taarifa, huku Thee Pluto akisisitiza haja ya kunyamaza na Felicity akitoa mtazamo wake kuhusu hali hiyo.

Ripoti zinaonyesha kuwa kutoelewana na kuvunjika kwa mawasiliano kulichangia pakubwa katika kuvunjika kwa uhusiano huo.

Related Articles

Back to top button