Muziki

Tamasha la 23 la Sauti za Busara 2026 lafunguliwa

ZANZIBAR: TAMASHA la 23 la Sauti za Busara linatarajiwa kuanza Februari 6 hadi 8, 2026, katika Mji Mkongwe wa kihistoria wa Zanzibar.

Tamasha hilo hufanyika kila mwaka likiadhimisha muziki na utamaduni wa Kiafrika kutoka mataifa mbalimbali duniani wakiadhimisha katika onesho zuri la talanta, umoja, na urithi wa utajiri wa bara la afrika.

Kwa miaka mingi, sauti za busara imeshirikisha zaidi ya bendi 460 kutoka zaidi ya nchi 60, zinazofanya muziki wa Taarab, Jazz hadi Afrobeats, Reggae, Hip-Hop, na Electronica.

Tamasha hilo linasisimua kwa programu mbalimbali za muziki wa live na limetambuliwa na mashirika kadhaa ya kimataifa kuwa ni mojawapo ya matamasha ya muziki bora na linaloheshimika zaidi barani Afrika

Katika tamasha la mwakani 2026 zaidi wasanii 400 wanatarajiwa kushiriki kutoka kote duniani wakionesha mchanganyiko wa muziki wa kitamaduni na wa kisasa wa Kiafrika.

Maonesho ya tamasha hilo yamepangwa kufanyika katika majukwaa tofauti yatakayopambwa na wasanii kadhaa ndani ya Mji Mkongwe,
likiwemo jukwaa kuu na kumbi za ziada za Forodhani na Fumba Town.

Tamasha hilo kila mwaka huanza na Gwaride la Kanivali, gwaride zuri la barabarani linalo jumuisha picha za kupendeza, mavazi ya kitamaduni, na muziki wa kusisimua.

Gwaride hilo litapita mitaa ya Mji Mkongwe, ikiunganisha kwa karibu na wenyeji na kutoa fursa za kupiga picha na wasanii mbalimbali.

Pia katika tamsha hilo kutakuwa na Jukwaa la Shakers: Jukwaa hili litawaleta pamoja wasanii, ili kueleza changamoto na kupata majibu kutoka kwa walengwa na pia litawaonesha namna ya kuondokana na changamoto hizo kwa lengo la kuwa na mafanikio zaidi katika kazi zao.

Related Articles

Back to top button