Muziki

at Joe: Kendrick Lamar, SZA ndio Ja Rule na Ashanti wapya

NEW YORK : NGULI wa Hip Hop Fat Joe amesema ushirikiano wa wanamuziki Kendrick Lamar na Solána Rowe maarufu SZA una mvuto katika muziki kama walivyokuwa wanamuziki Jarule na Ashant.

Wanamuziki hao wanatamba na wimbo ‘Doves in the Wind’ wa 2017, ‘Luther’ na ‘Gloria’ zilizopo katika LP ya Kendrick ‘GNought of all time’ ya Kendrick.

Akiongea kwenye podikasti yake ya ‘Joe na Jada’, Fat Joe amesema: “Usichojua ni kwamba hawa watakuwa marafiki wakubwa milele. Hivi sasa, wamepata takriban nyimbo sita au saba. Na zote ni namba moja. Wanaweza kuchukua asilimia 100. Wote wakali.”

Ameongeza: “Nawaita Ja na Ashanti kwa kuwa ndiyo wanamuziki wawili wakubwa zaidi wa wakati wote, walioshirikiana vyema na SZA na Kendrick ni kama wao.”

SZA hivi karibuni alisema anataka kufanya albamu kamili na mkali wa rap kwa sasa Kendrick Lamar.

SZA: “Ningependa kufanya albamu kamili na Kendrick Lamar. Nafikiri hilo lingekuwa jambo la kushangaza. Yeye ni rapa mkali napenda namna ambavyo anapokelewa kwa namna tofauti tofauti katika muziki wake.”

Alieleza: “Sijui kinachoendelea hata wewe hujui kinachoendelea. “Wakati ‘Luther’ alipotoka, nilisema, ‘Sawa, hiyo ndiyo sauti tunayotumia, kipindi.’ Sawa na ‘Gloria.’ Nikasema, ‘Sawa.’”

Wawili hao walianza safari yao ya ‘Grand National Tour’ mwezi Aprili, huku mbio hizo zikitarajiwa kukamilika Agosti 9 mwaka huu 2025.

Related Articles

Back to top button