EPL

Slot amtafakari TAA

LIVERPOOL: KOCHA wa mabingwa wapya wa ligi kuu ya England Liverpool, Arne Slot amesema bado hajaamua iwapo beki wake Mwingereza Trent Alexander-Arnold atakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mchezo wa ‘tandua jamvi’ wa ligi hiyo jumapoli dhidi ya Crystal Palace baada ya mchezaji huyo kuzomewa wiki mbili zilizopita

Alexander-Arnold ambaye alitangaza kuondoka Liverpool mkataba wake utakapomalizika mwisho wa msimu alikutana na hasira za mashabiki wa klabu hiyo walipoikaribisha Arsenal Anfield Mei 11 huku tayari kukiwa ripoti mbalimbali zilizohusisha beki huyo kumfuata swahiba wake Jude Bellingham Real Madrid.

“Inapaswa kuwa siku ambayo kila mtu anastahili kuifurahia. Imekuwa miaka 35 ambayo mashabiki wa Liverpool wamekuwa wakiusubiri sana wakati kama huu. Kila aliye ndani ya uwanja anastahili kuwepo, ikiwa ni pamoja na Trent, ambaye amekuwa sehemu ya msimu wa mafanikio na miaka yenye mafanikio katika klabu hii lakini bado sijaamua” Slot aliwaambia wanahabari.

Liverpool waliotwaa ubingwa wa ligi hiyo walipoichakaza Spurs 5-1 mwezi uliopita wataikaribisha Crystal Palace ambao bado wako kwenye sherehe za ubingwa wa kombe la FA, kombe lao la kwanza kubwa kwenye historia ya klabu hiyo ambako pia meneja wa zamani a Liverpool Juergen Klopp anatarajia kuwepo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button