La Liga

“Msinifananishe na messi” – Yamal

BARCELONA:KINDA wa FC Barcelona Lamine Yamal amesema amejikita zaidi kuwa yeye kuliko kujifananisha au kuwasikiliza wanaomfananishwa na Gwiji la soka na mchezaji bora mara 8 wa dunia Lionel Messi ambaye kwa sasa anakipiga kwenye Ligi kuu ya Marekani (MLS) akiwa na klabu ya Inter Miami.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa leo wa Nusu Fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Inter Milan, Yamal mwenye miaka 17 amesema iko wazi kuwa Messi ndiye mchezaji bora zaidi kwenye historia ya soka Duniani kwa sasa na yeye anamtazama kama mfano na si kujilinganisha nae.

“Sijilinganishi naye (Messi) kwa sababu sijilinganishi na yeyote acha Messi. Mara zote tunafikiria kujiimarisha zaidi na kuwa bora kesho zaidi ya jana kwahiyo sidhani hii milinganisho ina maana yeyote, akitajwa messi inakuwa upuuzi zaidi. Nitaendelea kufurahia kuwa mimi. Ni wazi kuwa namkubali sana kwakuwa ni mchezaji mkubwa kwenye historia lakini sijilinganishi nae” – amesema Yamal

Kinda huyo amekuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha Hansi Flick akikichafua kwenye mbavu ya kulia ambako mfungaji bora wa muda wote wa Barca Lionel Messi amekuwa akicheza kwa miaka mingi wotw wakiwa zao la academy ya klabu hiyo La Masia

Barcelona walifika hatua ya fainali ya Champions League wakiwa na Messi mwaka 2015 na Yamal ana matumaini makubwa ya kufanya hivyo kwa wacatalan hao msimu huu.

Related Articles

Back to top button