Son hataionja Liverpool, Europa fresh

LIVERPOOL:TOTTENHAM Hotspur watakuwa bila nahodha wao Son Heung-Min katika mchezo wao wa ugenini dhidi ya mabingwa watarajiwa wa ligi kuu ya England Liverpool lakini huenda akawa tayari kwa mchezo wa nusu fainali ya Europa League dhidi ya Bodo/Glimt Alhamisi Mei 8 mwaka huu.
Kocha mkuu wa kikosi hicho Ange Postecoglou amewaeleza hayo waandishi wa habari mapema leo alipokuwa akizungumzia maandilizi yao kuelekea katika mchezo huo wa Jumapili akisema kuwa Son ndiye mchezaji pekee atakayekosekana katika mchezo huo.
“Anaimarika na hilo ni jambo zuri, lakini hatakuwepo Jumapili tutaona iyo Alhamisi, ni kwa mara ya kwanza amegusa nyasi leo na nawahakikishia alikuwa bora kuliko alivyokuwa awali”
“Ni jeraha la mguu na kwakuwa miguu ndo inabeba mwili naona ni swala zuri kumpa muda zaidi apumzike. Tunaenda kupambana na kikosi bora zaidi, si vyema kuwaacha watutawale, tunaenda kupishana nao kwenye spaces” amesema Postecoglou
Son, raia wa Korea Kusini amekosa michezo mitatu iliyopita ya Tottenham kutokana na jeraha la mguu, tayari ni rasmi hataucheza mchezo dhidi ya Liverpool na madaktari wa timi hiyo wanapambana awepo kwenye mchezo wa Europa league.