Burudani

Gigy Money aonesha hisia zake kwa Diamond

DAR ES SALAAM:MSANII wa muziki wa kizazi kipya Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, ameweka ujumbe mzito akionyesha hisia zake kwa staa wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Katika ujumbe huo aliouweka kwenye akaunti yake ya Instagram Gigy aliandika: “Naapa, nimemuota Naseeb jana, mimi nmekumiss kichaa wangu. Ninachokijua tunapendana, mengine mtajijua, kikubwa tajiri hanuniwi,”

Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa, huku mashabiki wakijiuliza iwapo kuna uwezekano wa wawili hao kurudisha urafiki wao wa zamani au hata kushirikiana tena katika kazi za muziki.

Gigy aliendelea kueleza kuwa pamoja na kuwa si lazima wawe karibu kama zamani, bado ana mapenzi ya dhati kwa Diamond na kumuita “vibe la house party.”

Ameweka wazi kuwa hajawahi kuboreka wala kukerwa naye, huku akisema kuwa yeye(Gigy) ni “kipenzi cha wakaka wote Tanzania” na kuongeza kwa utani kuwa wasiotaka “wabishane na fuvu la kichwa chao.”

Hata hivyo, Diamond Platnumz hajatoa tamko lolote kuhusiana na kauli hiyo, lakini mashabiki wake na wa Gigy Money wanaendelea kufuatilia kwa karibu, huku wengi wakitarajia mawasiliano mapya au kolabo ya muziki kati yao.

Related Articles

Back to top button