Burudani

Doechii alimtosa mpenzi wake kisa albamu ya SZA

FLORIDA: RAPA kutoka Marekani Jaylah Hickmon maarufu Doechii ameweka wazi kwamba alilazimika kuachana na mpenzi wake kwa madai ya kuwa kikwazo katika albamu yake aliyoitoa mwaka 2017.

Mkali huyo wa wimbo wa ‘Anxiety’ amesema jamaa huyo alikuwa kikwazo katika kazi zake na hakuonesha kupenda sanaa ya muziki anayoifanya rapa huyo hivyo hakuona sababu ya kuendelea naye ingawa alimpenda.

“Nilihisi hivyo mara moja tu. Nilikuwa na umri wa miaka 18, na nilikuwa nachumbiana na mvulana ambaye hakuungwa mkono sana na muziki wangu, na ilinikandamiza mno. Niliacha hadi kuandika nyimbo zangu kwa sababu alikuwa akinikandamiza mno, ‘Hiyo sio sawa’.”

Doechi aliendelea “Nakumbuka nilisikiliza ‘Ctrl’ ya SZA kwa mara ya kwanza na ilinipa ujasiri wa kuachana naye. Nilizungumza tu kwa sababu alinikatisha tama kuhusu muziki wangu alisema nisingefika kokote na muziki wangu.”

Doechii aliandika wimbo wa kuachana kuhusu mpenzi huyo wa zamani. “Mwaka 2021, wimbo wa kwanza nilioutoa ambao ulienea sana, ulikuwa asilimia 100 kuhusu ex wangu huyo”.

Doechii ameeleza: “Nilikuwa nikifanya kazi kwa mwaka mmoja na nilimchezea, na alikuwa kama hapendi alikuwa akiniambia huu ni mbaya sijui hata unachozungumzia lakini wasichana waliupenda sana wimbo huo.

Related Articles

Back to top button