Kumbe Messi aliitamani tena Barca

BURNOS AIRES, MSHINDI mara 8 wa tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia Lionel Messi amefichua kuwa alikuwa na nia ya kurudi FC Barcelona alipoachana na mabingwa soka la Ufaransa PSG alikodumu kwa misimu miwili kabla ya familia yake kuamua gwiji huyo ajiunge na klabu ya Inter Miami ya nchini Marekani anayoitumikia hivi sasa.
Messi amefichua hayo katika mahojiano maalum na kipindi cha Televisheni cha Simplemente Fútbol cha nchi yake ya nyumbani Argentina. Ambapo Pamoja na mambo mengine amesema timu yake ya taifa kutawazwa kuwa mabibgwa wa Dunia ni jambo linguine liliochangia maamuzi ya yeye Kwenda Marekani.
“Nilikuwa na nia ya kurejea Barcelona, kuweza kurejea sehemu ambayo siku zote nilitaka kuwa, lakini haikuwezekana tena kutokana na hali ya klabu. Baada ya hapo, (kuchagua timu mpya) ikawa uamuzi wa familia. Halafu kuna ukweli kwamba tulishinda Kombe la Dunia, hii pia ilikuwa na mchango mkubwa. Ilikuwa wazi kwamba sitaki kuwa katika timu nyingine Ulaya, sikutaka kwenda kokote kati yao ” amesema Messi.
Messi ambaye kwa sasa anaenjoy mazingira mapya ya MLS na Inter Miami daima atakumbukwa kama gwiji wa FC Barcelona baada ya kuiacha klabu hiyo kwa hisia kali za huzuni mwaka 2021 na machozi yaliyojaa upendo kwa klabu hiyo na mashabiki wake.
Messi alisajiliwa na vigogo wa Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG) alikodumu kwa misimu miwili na kushinda mataji kadhaa kabla ya kufanya maamuzi yaliyoshtua wengi ya kutimkia MLS katika klabu ya Inter Miami ambako mpaka sasa ameshinda kombe la ligi na ngao ya jamii.




