Filamu

Van Damme atuhumiwa sakata la mapenzi

ROMANIA : Mcheza sinema Jean-Claude Van Damme ameingia katika Sakata la tuhuma za kutoka kimapenzi na Wanawake wanaosafirishwa kwa njia haramu.

Mcheza filamu huyo aliyewahi kutamba na filamu mbalimbali huku umahiri wake ukiwa katika matumizi ya mateke katika kupigana anahusika na malalamiko ya jinai yaliyowasilishwa na Kurugenzi ya Uchunguzi wa Uhalifu uliopangwa na Ugaidi wa Romania (DIICOT).

Nyota huyo mwenye miaka 64 anadaiwa kujihusiaha na mahusiano ya kimapenzi na wanawake ambao walikuwa wamesafirishwa na kundi la uhalifu linaloongozwa na Morel Bolea, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la CNN Antena 3.

Van Damme anatuhumiwa kupokea wanawake watano wa Kiromania kama zawadi huko Cannes, Ufaransa, kutoka kwa kikundi cha wafanyabiashara.

Wakili Adrian Cuculis, anayemwakilisha mmoja wa wahasiriwa, aliambia chombo hicho kuwa walikuwa katika hali ya hatari, kwa tuhuma kwamba walidhulumiwa kulingana na Kifungu cha 182 cha Sheria ya Jinai.

Aliongeza kuwa Warumi kadhaa ambao kwa sasa wanachunguzwa kwa kuunda kikundi cha uhalifu na ulaghai, wanadaiwa kumpa Jean-Claude Van Damme wanawake watano wa Kiromania, wanamitindo wa ili afanye nao ngono.

Mwanamke aliyeshuhudia tukio hilo anadaiwa kuzungumza na waendesha mashtaka, jambo lililosababisha DIICOT kufungua uchunguzi wa makosa ya jinai kama yapo.

Tukio hilo ni sehemu ya uchunguzi mkubwa zaidi wa usafirishaji haramu wa binadamu ambao Ofisi ya Mwendesha Mashtaka nchini Romania ilizindua mwaka wa 2020.

Kulingana na Antena 3, kwa sababu tukio linalodaiwa lilitokea Cannes, Mahakama Kuu ya Cassation nchini Ufaransa lazima iidhinishe kesi za jinai ili kesi hiyo isonge mbele.

Washukiwa hao wataitwa Romania kutoa maelezo. Wawakilishi wa Van Damme na DIICOT bado hawajatoa maoni yao kuhusu habari hizo.

Related Articles

Back to top button