Ligi Ya Wanawake

Mlandizi Queens hali ni mbaya

Yaruhusu magoli 70

DAR ES SALAAM:KATIKA timu 10 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake, Mlandizi Queens iko katika hali mbaya baada ya kuruhusu mabao 70 katika michezo 14 waliyocheza mpaka sasa.

Mlandizi Queens imekuwa timu ambayo kila mpinzani ameweza kuifunga mabao mengi, huku washambuliaji wakipata nafasi ya kufunga hat-trick moja au mbili katika mchezo mmoja.

Timu hiyo haijashinda mchezo hata mmoja msimu huu na inashika mkia kwa pointi moja pekee iliyopata kutokana na sare moja.

Kwa mwenendo huu, dalili zinaonesha kuwa Mlandizi Queens ina nafasi finyu ya kusalia kwenye ligi, kwani imebakiza michezo minne pekee kumaliza msimu, na kama itaendelea kupoteza, haitakuwa na nafasi ya kujinusuru kushuka daraja.

Kwa upande wa timu nyingine, Gets Program imeruhusu mabao 39, Ceasiaa Queens mabao 31, Alliance Girls mabao 25, Fountain Gate Princess na Bunda Queens mabao 20 kila moja, huku Mashujaa Queens ikiruhusu mabao 17.

Timu zilizoruhusu mabao machache ni kinara wa ligi JKT Queens, ambaye imefungwa mabao matatu pekee, Simba Queens mabao nane, huku Yanga Princess ikifungwa mabao 10.

 

 

 

Related Articles

Back to top button