Man City, Madrid uso kwa uso tena UCL

NYON: SIO huenda tena, sasa ni rasmi Mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya Real Madrid watakutana na mabingwa watetezi wa ligi ya England Manchester city katika playoff ya kuwania siti kwenye mitanange ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA champions league).
Mechi hiyo imethibitishwa mchana huu katika droo ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA iliyofanyika katika mji wa Nyon nchini nchini Switzerland

Manchester City na Real Madrid hawakuwa na mwanzo mzuri wa mashindano hayo ambayo sasa yanachezwa kwa mfumo wa ligi wakimaliza katika nafasi ya 11 na 22 na hatimaye wakajipata katika nafasi za nje ya kufuzu moja kwa moja kwa raundi ya 16 bora.
Mzunguko wa kwanza wa mchezo huu utapigwa Etihad tarehe kati ya tarehe 11 na 12 Februari kabla ya marudiano katika dimba la Santiago Bernabeu Februari 18 na 19. Hii ni mara ya 5 katika misimu 6 ya hivi karibuni vigogo hawa kukutana mara ya mwisho ikiwa katika nusu fainali ya michuano hii msimu uliopita na Man City waliondoshwa kwa penalti na Real Madrid wakawa mabingwa.
Mechi nyingine za playoffs ni kama ifuatavyo
Club Brugge v Atalanta
Sporting v Borussia Dortmund
Manchester City v Real Madrid
Celtic v Bayern Munich
Juventus v PSV Eindhoven
Feyenoord v AC Milan
Brest v Paris St Germain
AS Monaco v Benfica
Droo ya 16 bora itapangwa Februari 21





