EPL

Moyes arudi na moto Everton

LIVERPPOOL:Baada ya kutangazwa kama Kocha mpya wa Everton David Moyes amesema anafurahi kurejea klabuni hapo na yuko tayari kuibadilisha timu hiyo na kuirejesha katika makali yake kutokana na mwenendo mbaya wa klabu hiyo chini ya kocha Sean Dyche aliyetimuliwa juzi Alhamisi Januari 9, 2025.

Moyes mwenye miaka 61 amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu na anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuinasua Everton kutoka nafasi 16 kwenye msimamo na pointi 17 zilizopatikana kutokana na ushindi kwenye mechi 3 pekee huku wakiwa na sare 8 na vipigo 8 msimu huu

“Nina furaha kurejea hapa, sikusita kuchukua fursa ya kujiunga na klabu hii mara tu nilipotafutwa kwa sababu ni hapa nilipata mafanikio makubwa kwa miaka 11. Ninawaomba mashabiki wetu wasimame nasi, wawe nyuma ya wachezaji ili uwe msimu mzuri kwetu turejeshe klabu kwenye nafasi yake” amesema Moyes

Moyes aliwahi kuwa kocha wa Everton kuanzia 2002 hadi 2013 kabla ya kuwa kocha wa Manchester United, Real Sociedad ya Uhispania, Sunderland na West Ham mara mbili na amekuwa nje ya kazi tangu alipotwaa ubingwa wa Europa Conference League mwaka 2023 akiwa na West Ham.

Related Articles

Back to top button