EPL

Alexander Isak ampiku Salah tuzo za mwezi

MSHAMBULIAJI wa Newcastle, Alexander Isak, ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mwezi Desemba.
 
Mshambuliaji huyo wa Sweden alifunga mabao manane na kutoa pasi mbili za mabao kwa Newcastle, ambao walishinda mechi nne kati ya sita za ligi walizocheza mwezi huo.
 
Isak pia alipata tuzo nyingine baada ya bao lake dhidi ya Liverpool kushinda Tuzo ya Bao Bora la Mwezi wa Ligi Kuu.
 
Kumeibuka gumzo kwa mashabiki wa soka baada ya kudai Mohamed Salah alistahili tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Desemba baada ya kuhusika katika mabao 14, akifunga 7 na kutoa pasi 7 za mabao.Idadi hiyo haijawahi kufikiwa na mchezaji yeyote zaidi ya Salah na Luis Suarez alipokuwa akiichezea Liverpool miaka ya nyuma.
 
Unadhani Salah ameonewa au Isak alistahili zaidi tuzo hiyo?

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button