Yanga kuwapa mashabiki furaha leo?

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga leo inashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Hilal ya Sudan.
Kwa wiki kadhaa mashabiki wa Yanga wamesubiri mchezo huo huku viongozi wa klabu hiyo wakiwahamasisha kuwapa waboti wachezaji.
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazungira mazuri ya kufuzu kwenda hatua ya makundi kabla ya mchezo wa marudiano Oktoba 16 huko Sudan.
Michezo mingine ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayopigwa leo ni kama ifuatavyo:
Rail Club du Kadiogo vs AS Vita Club
ASKO vs JS Kabylie
ASN Nigelec vs Raja Casablanca
Cape Town City vs Petro Atletico