
ZURICH: Timu ya taifa ya England na ya Serbia zitakutana tena uso kwa uso katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia la 2026 nchini Marekani baada ya droo ya michuano hiyo kuwekwa hadharani leo mjini Zurich nchini Switzerland.
England na Serbia walitoa mchezo mzuri kwenye hatua ya makundi ya michuano ya Euro 2024 na Serbia ilipotea kwa 1-0, hivyo Serbia wanayo nafasi ya kulipiza kisasi.
Hata hivyo, timu nyingi zipo gizani juu ya wapinzani wao kwenye makundi kwa sababu ya droo hiyo imefanyika ikiyaacha makundi manane yakiwa hayajaamuliwa kikamilifu kwani yatakamilishwa na washindi au walioshindwa katika robo fainali ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya, itakayofanyika Machi mwakani.
England ni mojawapo ya nchi nne zinazofahamu wapinzani wao kikamilifu na chini ya meneja mpya Thomas Tuchel, ambaye atachukua usukani kuanzia Januari 1, watamenyana na Serbia, Albania, Latvia na Andorra katika Kundi K.
Kwenye Euro 2024, Uingereza iliifunga Serbia bao 1-0 katika mchezo wao wa ufunguzi wa makundi kabla ya kutinga fainali ambayo walifungwa 2-1 na Hispania.
Hispania wao watamenyana na Uholanzi katika robo fainali ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya, na mshindi ataungana na Uturuki, Georgia na Bulgaria katika Kundi E huku timu iliyopoteza ikiingia Kundi G pamoja na Poland, Finland, Lithuania na Malta.
Wanafainali wa Kombe la Dunia 2022 Ufaransa walio pia katika robo fainali ya Ligi ya Mataifa ulaya dhidi ya Croatia, na wakishinda hilo wataingia Kundi D pamoja na Ukraine, Iceland na Azerbaijan.
Kombe la Dunia la 2026 litachezwa nchini Marekani, Canada na Mexico, likianza Juni 11 na fainali Julai 19, na litakuwa la kwanza kujumuisha timu 48, ikiongezwa kutoka 32.
Group A
Mshindi kati ya Ujerumani/Italy
Slovakia
Ireland kaskazini
Luxembourg
Group B
Switzerland
Sweden
Slovenia
Kosovo
Group C
Atayepoteza kati ya Ureno/Denmark
Ugiriki
Scotland
Belarus
Group D
Mshindi kati ya Ufaransa/Croatia
Ukraine
Iceland
Azerbaijan
Group E
Mshindi kati ya Hispania/Uholanzi
Uturuki
Georgia
Bulgaria
Group F
Mshindi kati ya Ureno/Denmark
Hungary
Ireland
Armenia
Group G
Atakayepoteza kati ya Hispania/Uholanzi
Poland
Finland
Lithuania
Malta
Group H
Austria
Romania
Bosnia
Cyprus
San Marino
Group I
Atakayepoteza kati ya Ujerumani/Italy
Norway
Israel
Estonia
Moldova
Group J
Belgium
Wales
Macedonia kaskazini
Kazakhstan
Liechtenstein
Group K
England
Serbia
Albania
Latvia
Andorra
Group L
Atayepoteza kati ya Ufaransa/Croatia
Czech Republic
Montenegro
Faroe Islands
Gibraltar
Mechi hizi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 zitapigwa mwezi Machi mwakani na zitaendelea hadi November kila timu ikicheza nyumbani na ugenini.




