Ligi Daraja La Kwanza

Baraza atajwa tajwa Mtibwa

DAR ES SALAAM: WAKATI uongozi wa Mtibwa Sugar ukisaka kocha mpya, imeelezwa kuwa Mkenya, Francis Baraza ni miongoni mwa walimu wanaotajwa kuchukua nafasi ya Melis Medo aliyetimikia Kagera Sugar.

Imeelezwa kuwa uamuzi wa viongozi kumtaka Baraza ni kuendelea kutafuta matokeo mazuri katika ligi ya Championship na kuchukua nafasi ya Medo kuachana na wakata miwa wa Manungu na kutimkia Kagera Sugar inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Spotileo ilimtafuta, Kocha Baraza kuzungumzia uvumi huo na kuweka wazi kuwa hakuna kiongozi aliyemfuata kuhitaji huduma yake ya kufundisha klabu hiyo.

“Ni kweli nipo Tanzania nimeingia jana usiku, nimekuja kwa ajili ya kuangalia fainali ya CECAFA, suala la kutakiwa Mtibwa Sugar hakuna kiongozi aliyenifuata, wakija mezani nipo tayari kufundisha,” amesema Baraza.

Mtibwa Sugar inayoshiriki ligi ya Championship, imedhamilia kufanya vizuri katika michuano hiyo kwa lengo la kurejea kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu wa 2024/25.

Related Articles

Back to top button