Africa

Wapinzani wa Simba, Yanga CAF usipime

HATUA ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ile ya Kombe la Shirikisho, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kati ya Februari 10 na 11 mwakani huku Tanzania ikiwakilishwa na Simba na Yanga.

Simba ambayo itaiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa imepangwa kundi C na timu za
Raja Casablanca ya Morocco, Horoya ya Guinea na Vipers ya Uganda.

Wekundu wa Msimbazi wameweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza nchini Tanzania kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku mara mbili ikiishia robo fainali msimu wa mwaka 2018/19 na 2020/21.

Msimu wa mwaka 2018/19 ilipangwa kundi D, na Al Ahly, JS Saoura na As Vita ambapo Simba ilimaliza katika nafasi ya pili ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda mara mbili sare mbili na kupoteza michezo miwili na hivyo kusonga mbele.

Mwaka 2020/21 ilipangwa kundi A na Al Ahly, As Vita na Al Merrikh, Simba ilimaliza ikiwa
kileleni mwa msimamo baada ya kujikusanyia pointi 14 ikishinda mara nne sare moja na kupoteza mchezo mmoja.

Wakati mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga inakuwa mara ya tatu kucheza hatua ya
makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ikifanya hivyo mwaka 2016 wakati mfumo ulipokuwa na makundi mawili yenye timu nne huku ikirudia tena mwaka mwaka 2018 zilipokuwa timu 16 zilizogawanywa makundi manne.

Mwaka 2016 ilikuwa kundi A na TP Mazembe, Mo Bejaia na Medeama ambapo Yanga ilimaliza hatua ya makundi ikiwa nafasi ya nne ikimaliza na pointi nne ikishinda mchezo mmoja sare moja kupoteza michezo minne.

Mwaka 2018, Yanga ilikuwa kundi D, na USM Alger, Rayon Sports na Gor Mahia mabingwa
hawa watetezi wa Ligi Kuu Bara walimaliza hatua ya makundi wakiwa nafasi ya nne baada ya kujikusanyia pointi nne ikiwa imeshinda mchezo mmoja sare moja na kupoteza michezo minne.

Wafuatao ni wapinzani wao wanaoenda kukutana nao ili kutafuta nafasi ya kupenya hatua
ya robo fainali ya mashindano ya CAF msimu huu.

RAJA CASABLANCA
Moja ya timu bora kutoka Morocco, ambayo imejipambanua kuwa timu kubwa Afrika
ilianzishwa mwaka 1949 ikiwa imetimiza miaka 73 hadi sasa.

Rais wa klabu hiyo ni Aziz El Badraoui huku kocha mkuu akiwa ni Mondher Kebaier, ambaye aliiongoza kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Morocco nyuma ya Wyadad AC msimu uliopita.

Miamba hii ambayo inapendelea kutumia rangi nyeupe na kijani ambazo zinaashiria kuwa na matumaini imewahi kutwaa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1989, 1997, 1999 huku ikiwa imeshinda taji la Shirikisho mara mbili mwaka 2018 na 2021.

Kikosi chao kina wachezaji 32 ambao umri wao wastani ni asilimia 25, kati yao sita ni nyota
wa kigeni.

Miamba hiyo inatumia Uwanja wa Mohamed V, wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 45,000 huku kikosi chao kikiwa na thamani ya Euro milioni 15.24 ambazo ni sawa na Sh bilioni 36.74 za kitanzania.

Nyota wa kuangaliwa ni Mohamed Nahiri, ambaye hadi sasa amepachika mabao manne kwenye chati ya wafungaji kwenye Ligi Kuu ya Morocco Botola Pro.

HOROYA AC
Mimba mingine kutoka Guinea ni miongoni mwa timu zinazoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, haijawahi kutwaa taji hili mafanikio yake makubwa ni kucheza robo fainali
mwaka 2018 na 2019 .

Kikosi chao kina wachezaji 31 wastani wa umri wao ni miaka 26, kina wachezaji 12 wa kigeni kutoka mataifa tofauti Afrika. Miamba hiyo kikosi chao kina thamani ya Euro milioni 1.23 sawa Sh Bilioni 3 za Kitazania.

Wanatumia Uwanja wa Stade du 28 Septembre ambao una uwezo wa kuchukua watazamaji elfu 25.000.

VIPERS
Ikiwa ndio mara yao ya kwanza kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa
ndio mafanikio yao makubwa katika ngazi ya kimataifa. Kikosi chao kina wachezaji 29, wachezaji wa kigeni wakiwa wanne thamani yao ni Euro 725,000, ambazo ni sawa na Sh
1.7 bilioni ambayo ni ndogo kuliko timu zote za kundi D.

Mabingwa hawa wa Ligi Kuu ya Uganda wanatumia Uwanja wa St. Mary’s Stadium Kitende
ambao unachukua watazamaji 25.000 waliokaa vitini.

Nyota wa kuchungwa ni mshambuliaji wake kinara Yunus Sentamu, ambaye ni kinara kwenye orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu ya Uganda hadi sasa akiwa amepachika mabao sita.

TP MAZEMBE- DR CONGO
Mpinzani mwenye mzani mzito zaidi kwenye kundi D ni TP Mazembe. Hawa ni mabingwa
mara 5 wa Ligi ya Mabingwa, Bingwa mara 2 wa Kombe la Shirikisho Afrika. Mazembe wako kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Vipers SC kutoka Uganda.

Thamani ya kikosi chao kwa sasa kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Market ni Dola za Marekani milioni 1.8, ni zaidi ya Sh Bilioni 4.2 za Kitanzania. Wanatumia uwanja wao wa
nyumbani, mjini Lubumbashi na una uwezo wa kuchukua watazamaji 18,500.

US MONASTIR
Ni klabu ya muda mrefu nchini Tunisia, ilianzishwa mwaka 1923, miaka 99 iliyopita. Hii ni
mara ya kwanza kushiriki hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF.

Licha ya uchanga wao kwenye kundi hili, ni timu yenye msuli mkubwa zaidi wa kiuchumi,
thamani ya kikosi chao ni Dola za Marekani Milion 9.5( zaidi ya Sh Bilioni 22 za Tanzania).

Wanaingia makundi kifua mbele baada ya kuwatoa mabingwa watetezi wa Kombe hili, RS
Berkane kutoka Morocco.

Sehemu ya wachezaji wa kikosi cha AS Real Bamako ya Mali.

REAL BAMAKO

Timu ya tatu kwa mafanikio nchini Mali nyuma ya Stade Malien na Djoliba AC. Ilikua tishio
mwanzoni mwa miaka ya 90, ikibeba Ubingwa wa Ligi Kuu mara 6 na kombe la ligi mara 9.

Wakaenda CAF wakacheza fainali ya Klabu Bingwa Afrika 1966 walipoteza kwa Stade
Abidjan ya Ivory Coast. Baada ya kuona soka la Mali haliwalipi wakabadilisha maisha chini ya raisi wao Famakan Dembele.

Wakaamua kuifanya klabu ya kukuza vipaji na kuuza kwa ushirikiano na JMG aliyejenga
kituo cha Asec Mimosas ya Ivory Coast, Moja ya nyota waliopita ni Semasekou wa Hoffenheim, Mohamed Camara wa Monaco na Yves Bissouma wa Tottenham Hotspurs.

Related Articles

Back to top button