Muigizaji atafuta bodyguard baada ya kuchomwa visu

CHENAI: MUIGIZAJI wa India Saif Ali Khan amesema baada ya kunusurika katika shambulio la visu mwezi Januari nyumbani kwake ndicho kilichomlazimu kuweka walinzi wa kumlinda ingawa hajazoea mazingira ya kulindwa lindwa.
Muigizaji huyo anadaiwa kuchomwa kisu na Shariful Islam, ambaye alikamatwa na polisi baada ya jaribio hilo la ujambazi. Baada ya shambulio hilo, kipande cha kisu kilitolewa kwenye mgongo wa mwigizaji huyo, pamoja na majeraha mengine alifanyiwa upasuaji mara mbili na alipotoka salama chumba cha upasuaji akaajili walinzi wa kumlinda yeye na usalama wake.
Akizungumza na ETimes, Seif alifunguka kuhusu tukio hilo la kutisha na jinsi lilivyomfundisha kuwa mwangalifu kuhusu kufunga milango na madirisha ya nyumba yake.
Muigizaji huyo wa ‘Love Aaj Kal’ amesisitiza kwamba kila mtu anapaswa kuimarisha usalama wake na kuwa na walinzi si ufahali kama wengi wanavyodhani.
Muigizaji huyo, hata hivyo, alisisitiza kwamba ingawa anajali sana usalama wake na familia yake baada ya shambulio hilo, hajawahi kuamini katika walinzi hapo awali.
Seif hivi karibuni alinunua nyumba iliyopo Doha, Qatar. Na aliwaambia waandishi wa habari kuwa nyumba hiyo ni salama kwa kuwa ina walinzi wa kutosha.
Alisema, “Moja ni kwamba haiko mbali sana na inafikika kwa urahisi. Na kisha jambo lingine ni kwamba, jambo la muhimu zaidi ni kwamba ni salama sana.”




