Muziki

Zuchu kunogesha fainali za CHAN 2024

DAR ES SALAAM: MWANAMUZIKI wa muziki wa Bongo Fleva, Zuhura Othman ‘Zuchu’, anatarajiwa kutoa burudani katika Fainali za mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024).

Fainali hizo zitakazohusisha timu ya Morocco dhidi ya Madagascar zitarajiwa kuchezwa Jumamosi Agosti 30, 2025 kwenye Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi nchini Kenya.

Zuchu ameweka ujumbe kwenye mtandao wake wa kijamii juu ya fursa hiyo aliyopata akionesha furaha yake kubwa kwani itamuweka mbele ya maelfu ya mashabiki wa soka barani Afrika.

“Nina furaha kutangaza kuwa nitakuwa miongoni mwa wasanii watakaoimba kwenye fainali za Chan mwaka huu,”

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), sherehe za kufunga mashindano hayo zitajumuisha muziki, tamaduni na burudani zenye kuonesha upekee wa bara la Afrika.

Related Articles

Back to top button