Zee Cuty afunguka kuteswa Kisaikolojia

MSANII maarufu wa muziki Zee Cuty ameweka wazi hali yake ya kisaikolojia kwa sasa, akieleza kuwa anapitia kipindi kigumu cha msongo wa mawazo na anahitaji msaada ili kuimarika.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, msanii huyo alieleza wazi kuwa hali yake si nzuri kwa sasa kutokana na changamoto mbalimbali anazokabiliana nazo.
Pamoja na hilo, aliwaasa wasanii chipukizi na wale wanaotamani kuingia kwenye tasnia ya muziki kutambua kuwa safari ya muziki si rahisi kama wengi wanavyodhani.
“Nawashauri wote wenye ndoto ya kuingia kwenye muziki, wajiandae kupambana kwa bidii, kwa sababu si jambo rahisi. Changamoto ni nyingi na zinahitaji nguvu ya akili na moyo,” aliandika Zee Cuty.
Mashabiki wake na wadau mbalimbali wamemiminika kwenye ukurasa wake wakimpa pole na kumuombea apate nafuu haraka.