EPL

Yoro atabiri ‘ufufuko’ wa Manchester United msimu huu

MANCHESTER: KWA beki chipukizi Leny Yoro na wenzake Manchester United, mchezo wa Jumamosi dhidi ya Tottenham Hotspur hautakuwa tu mechi nyingine ya Ligi Kuu ya England bali ni nafasi ya kufuta kumbukumbu chungu ya kipigo cha fainali ya Ligi ya Europa msimu uliopita.

United walipoteza kwa bao 1–0 dhidi ya Spurs katika fainali iliyochezwa mjini Bilbao, matokeo yaliyowanyima nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu huu na kuweka doa kwenye msimu uliokuwa tayari mbaya zaidi katika historia ya klabu hiyo kwenye EPL.

“Kila mtu anajua kilichotokea kwenye fainali. Kwa hiyo naamini mechi hii ni nafasi nzuri kwetu kuthibitisha kuwa matokeo yale yangekuwa tofauti.” – amesema Yoro, mwenye umri wa miaka 19.

Yoro, aliyesajiliwa akitokea Lille kwa matarajio makubwa, alikiri kuwa kufungwa kwenye fainali kulikuwa pigo, lakini akasema kuna upande mzuri kwani kukosa michuano ya Ulaya kumeipa timu muda zaidi wa maandalizi.

“Bila shaka kila mchezaji anataka kucheza Ligi ya Mabingwa,” alisema. “Lakini kwa sasa tunacheza mechi moja kwa wiki, jambo lililotusaidia kuboresha yale ambayo hayakuwa mazuri msimu uliopita.”

United wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa hawajapoteza katika mechi nne mfululizo, na wanashika nafasi ya nane wakiwa pointi mbili tu nyuma ya Manchester City wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Licha ya maumivu ya kumaliza nafasi ya 15 msimu uliopita, Yoro amesema hakuwahi kujutia uamuzi wake wa kujiunga na Manchester United. Msimu huu, timu hiyo imekuwa na muda zaidi wa kufanya mazoezi na kuboresha mbinu mpya chini ya kocha Ruben Amorim, ambaye amekuwa akibadilisha mara kwa mara mabeki wake wa kati.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button