Nyumbani

Yanga yamuuza Bangala Azam

KLABU ya Yanga imetangaza kumuuza mchezake wake Yannick Bangala katika timu ya Azam.

Bangala hakuwemo kwenye utambulisho wa wachezaji katika kilelele cha Wiki ya Mwananchi Julai 22, 2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Uongozi wa Young Africans SC unapenda kuutarifu Umma kuwa tumefikia makubaliano na Klabu ya Azam FC kumnunua mchezaji wetu Yannick Bangala,” imesema Yanga kupitia mitandao yake ya kijamii.

Katika taarifa yake Azam imesema:”Tumefikia makubaliano na klabu ya Yanga ya kumnunua, mchezaji kiraka, @ybangala4 na amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufuzu vipimo vya afya.”

Bangala anakuwa mchezaji wa pili Yanga kumuuza Azam katika siku za hivi karibuni baada ya Feisal Salum kusaini kuwatumikia matajiri hao wa Chamazi Juni 8 mwaka huu.

Related Articles

Back to top button