Ligi KuuNyumbani

Yanga vs Singida BS mechi ya siku

LIGI Kuu ya soka Tanzania inaendelea leo kwa michezo 3 kufanyika viwanja tofauti huku mchezo wa Yanga dhidi ya Singida Big Stars ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki.

Yanga inaikaribisha Singida BS uwanja wa Bemjamin Mkapa Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa mwisho leo.

Yanga inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 baada ya michezo 9 wakati Singida BS ipo nafasi ya 4 ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 10.

Katika mchezo wa mapema mchana Polisi Tanzania itakuwa mgeni wa Ihefu katika uwanja wa Highland Estates uliopo Mbarali mkoani Mbeya.

Polisi Tanzania inashika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 11 wakati Ihefu ni ya mwisho nafasi ya 16 ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 10.

Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya utashuhudia mchezo mwingine wa ligi Mbeya City ikiwa mwenyeji wa Kagera Sugar.

Mbeya City ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 16 baada ya michezo 10 wakati Kagera Sugar ni 12 ikiwa imejikusanyia pointi 11 baada ya michezo 11.

Related Articles

Back to top button