Africa

Yanga kuifuata Rivers Aprili 20

KIKOSI cha timu Yanga kitaondoka Dar es Salaam Aprili 20 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United ya nchi hiyo Aprili 23.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Godswill Akpabio uliopo mji wa Uyo katika jimbo la Akwa Ibom Kusini mwa Nigeria.

Afisa habari wa Yanga Ally Kamwe amesema wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na hakuna majeruhi kasoro Aboutwalib Mshery mwenye majeraha na Mamadou Doumbia aliyepata msiba wa baba yake mzazi ambaye atakuangana na timu Addis Ababa, Ethipia.

“Tarehe 23 tunakwenda kucheza mchezo mkubwa na muhimu kwenye historia ya Klabu yetu ugenini, tunawaomba Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Young Africans SC kuiombea Klabu yetu iweze kufanya vizuri kwenye mchezo huu muhimu wa kwanza wa robo fainal,i” amesema Kamwe

Mchezo wa marudiano wa Yanga dhidi ya Rivers United utachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 30, 2023.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button