
BAADA ya ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Singida Big Stars Novemba 17 Yanga leo inashuka dimbani kuivaa Dodoma Jiji katika mfululizo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.
Mchezo huo pekee leo utafanyika uwanja wa Liti mjini Singida.
Yanga inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 26 baada ya michezo 10 wakati Dodoma Jiji ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 11.