Yanga kamili yaifuata US Monastir

KIKOSI cha watu 31 wakiwemo wachezaji na benchi ufundi kinaondoka leo alasiri kwenda Tunisia kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya US Monastir ya nchi hiyo Febriari 12.
Afisa habari Yanga Ally Kamwe amewataja wachezaji hao kuwa magolikipa ni Djigui Diarra, Metacha Mnata na Erick JOhola.
Mabeki ni Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrihim Abdullah(Bacca), Wadol Shabani Djuma, Kibwana Shomari, Mutambala Lomalisa, Mamadou Doumbia na David Bryson.
Viungo ni Khalid Aucho, Yannick Bangala, Zawadi Mbuya, Mudathir Yahya, Salum Abubakar, Farid Mussa, Dickson Ambundo, Jesus Moloko na Kisinda Twisila.
Amewataja washambuliaji kuwa ni Stephane Aziz Ki, Clement Mziza, Kennedy Musonda na Fiston Mayele.
“Tunaondoka Dar Es Salaam leo saa 9:25 alasiri kuelekea Dubai, ambapo tutapumzika hapo na kesho tutaondoka kuelekea Tunisia, tunasafiri na wachezaji 25 na benchi la ufundi 6 pamoja na Aboutwalib Mshery akienda kwa ajili ya matibabu na Mwalimu Nabi akiwa ameshatangulia Tunisia kwa ajili ya maandalizi,”amesema Kamwe.
Yanga ipo kundi D ambapo timu nyingine ni TP Mazembe ya Jamhuri ya Kimokrasi ya Congo na AS Real Bamako ya Mali.