Africa

Yanga bungeni tena

UKUBWA na ubora wa Yanga unaendelea kuonekana kwenye kila kona nchini, baada ya  jana timu hiyo kutawala bungeni jijini Dodoma leo hii simulizi ya timu hiyo nchini inaendelea kutawala bungeni.

Akizungumza wakati  wa kipindi cha maswali majibu ,Waziri Mkuu, Kassim majaliwa ameipongeza timu hiyo kwa kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa baada ya jana kutakata kwenye Dimba la Benjamini Mkapa kwa kuisulubisha Marumo Gallants bao 2-0 kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

’Hakika Dar Young Africans inaendelea kupuperusha vyema bendera ya Tanzania , na niwapongeze sana kwa maatokeo ya jana, tunawaombea sana kwa mchezo wa marudiano kule Afrika kusini mshinde kwa magoli mengi, watanzania tuna hamu ya kuona tukishiriki fainali” alisema Waziri mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema taifa linajivunia ubora wa timu hiyo na Imani yao ni kwamba bendera ya taifa itaendelea kuwakilisha vyema na mabingwa hao wa soka la bongo, Aidha Waziri mkuu amesema shauku ya serikali ni kuiona timu hiyo ikicheza fainali ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika.

Related Articles

Back to top button