Kwingineko

Yamal ang’ara tuzo za Globe Soccer

DUBAI:FC Barcelona na Paris Saint-Germain ndizo klabu zilizotawala tuzo za Globe Soccer Awards zilizofanyika Dubai, huku macho yote yakielekezwa kwa kinda wa Barcelona, Lamine Yamal, aliyeibuka nyota wa usiku huo.
Yamal, ambaye bado ni kijana mdogo , alikusanya tuzo tatu kubwa ambazo ni Mchezaji Bora wa chini ya umri wa miaka 23 LaLiga, Mshambuliaji Bora wa Mwaka, pamoja na Tuzo maalumu ya Maradona inayotolewa kwa kipaji bora chipukizi duniani. Mafanikio hayo yalimfanya azungumziwe zaidi kuliko mtu yeyote kwenye hafla hiyo.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo, Yamal alisema msimu uliopita alikuwa bado mtoto anayeanza, lakini sasa anahisi uzito wa kuwa mchezaji muhimu kwa klabu na timu ya taifa. Aligusia pia suala la kulinganishwa na mastaa wakubwa kama Cristiano Ronaldo, akisema ni bora kila mchezaji awe yeye mwenyewe, kwa sababu hata Ronaldo alifanikiwa kwa kuwa aliamini njia yake.
Usiku huo haukuwa wa Yamal pekee kwa Barcelona. Aitana Bonmatí alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike wa Mwaka, Raphinha akachukua tuzo ya Mchezaji Bora LaLiga, huku Hansi Flick akitangazwa Kocha Bora wa ligi ya Hispania. Barcelona pia ilitunukiwa tuzo ya Timu Bora ya Hispania pamoja na Klabu Bora ya Wanawake.
Kwa upande wa PSG, Ousmane Dembélé alitangazwa Mchezaji Bora wa Kiume wa Mwaka, huku klabu hiyo ya Ufaransa ikitwaa tuzo ya Klabu Bora ya Wanaume, ikiwa ni mara yao ya kwanza kushinda heshima hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button