EPL

Wolves yamnasa mkimbiza upepo wa Serie A

NAPLES: KLABU ya Ligi Kuu ya England Wolverhampton Wanderers (Wolves) wamemsajili Beki wa Cameroon Jackson Tchatchoua anayesifiwa kuwa mchezaji mwenye kasi zaidi kwenye Serie A msimu uliopita kutoka Hellas Verona ya Italia kwa mkataba wa miaka mitano.

Wolves imesema dili la beki huyo wa kulia mzaliwa wa Ubelgiji linajumuisha chaguo la kurefusha mkataba huo kwa miezi 12. Kitengo cha michezo cha Shirika la Habari la BBC kimeripoti kuwa dili hilo limeigharimu Wolves euro milioni 12.5.

Tchatchoua alirekodi kasi ya juu ya kilomita 36.3 msimu uliopita, kwa mujibu wa klabu hiyo, na alifunga mabao mawili na asisti tatu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ni mchezaji mpya wa nne wa Wolves katika dirisha hili la usajili.

Taarifa ya klabu hiyo imemnukuu Tchatchoua akisema kucheza katika Ligi ya England ni moja ya ndoto zake na ni hatua moja ambayo alitaka kuipiga katika maisha yake lakini pia maevutiwa pia historia ya klabu hiyo, uwanja, Pamoja na mashabiki .

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button