Filamu

Washindi mbio za Ngalawa hawa hapa

ZANZIBAR: KAMPUNI ya Rais ndiyo iliyoibuka kidedea katika mbio za Ngalawa ikizishinda Azam Media na Batista pamoja na ngalawa nyingine zaidia ya 10 zilizoshiriki katika mbio hizo zilizoandaliwa na Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF) 2025.

Mbio hizo zilifanytika katika fukwe ya Serena bahari ya Hindi ambapo resi hizo zilizomalizika kwa mafanikio, huku Ngalawa yenye jina la Rais ikifika ya kwanza na kuibuka na kitita cha fedha na zawadi nyingine.

Ngalawa ya Batista ilishika nafasi ya pili huku Ngalawa ya Azam Media ikishika nafasi ya tatu washindi watatu katika mashindano hayo ndiyo waliibuka na kitita cga fedha na zawadi nyingine na washiriki wengine wanasubitri mashindano ya mwakani ili nao wafanye vizuri na kujizolea zawadi mbalimbali.

Resi za ngalawa zina historia ndefu na tajiri hapa Zanzibar, zikiwakilisha urithi wa bahari na ufundi wa wavuvi wa eneo hili.

Kwa karne nyingi, ngalawa zimetumika kama vyombo muhimu vya uvuvi na usafiri kati ya visiwa, na mashindano ya ngalawa yamekuwa sehemu ya jadi ya jamii, yakionyesha ustadi wa manahodha na uwezo wa kudhibiti upepo na mawimbi.

Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF), Joseph Mwale amethibitisha kuwa tamasha hilo litaendelea kuenzi na kukuza tamaduni za Zanzibar, ikiwemo resi za ngalawa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button