Burudani

Wasanii binafsi, MCz, Djz kunufaika na ada mpya za  usajili Basata

DODOMA: WAZIRI wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya maboresho ya kurekebisha, kuanzisha, kufuta au kupunguza ada na tozo mbalimbali zinazotozwa na Wizara, Idara na Taasisi zinazojitegemea ili kuleta usimamizi bora wa sekta mbalimbali na kuboresha mazingira ya biashara nchini.

Hatua hizi ni moja ya sehemu ya mwendelezo wa utekelezaji wa Mpango wa kuboresha Mfumo wa udhibiti wa Biashara (Blueprint for Regulatory Reforms to Improve the Business Environment).

Mapendekezo ya ada yaliyopendekezwa na kukubaliwa kwa ada za huduma zinazotolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambazo zitalipwa mara moja tu ni kama ifuatavyo:

Msanii Binafsi au aliye kwenye kikundi atatozwa ada ya 10,000 badala ya ada ya awali ya 20,000, ili kuhamasisha wasanii wengi kujisajili mpaka wale wa vijijini nakuongeza urasimishaji wa sekta, jambo hilo limetokana na Kanuni za Baraza Kifungu cha 20 (a)-(b).

Mameneja wa Wasanii, Watozi (Producers), Wapigapicha za Mnato, Manjumuziki (DJs) na Waneni (MCs) watatozwa ada ya 10,000 ili kuongeza mapato ya Kanuni za Baraza Serikali na kurasimisha kazi zao, ili kuwawezesha kupata mikopo ya Serikali kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, jambo hilo limetokana na Kifungu cha 20 (a)-(b).

Wengine wanaonufaika na wasanifu wa Picha/matangazo (Graphics Designers) watatozwa 10,000 lengo ni Kuongeza mapato ya Serikali na kurasimisha kazi zao, ili kuwawezesha kupata mikopo ya Serikali kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Marekebisho ya Sheria ya Baraza Na. 5 ya 2019 Kifungu cha 17 (b) (i).

Mashirikisho ya Sanaa na vikundi vya Sanaa vitatozwa ada ya 30,000 huku Vyama vya Sanaa vitalipa ada ya 20,000 sababu kuu ya punguzo hilo ni kuwezesha mashirikisho na uanzishwaji wa vyama vingi vya sanaa na kupata wanachama wengi, hilo limefanyika chini ya  kanuni ya Barasa hilo kifungu cha 21 (1)-(4).

Wasanii wengine walionufaika ni Wapamb aji katika sherehe/ matukio watatozwa 10,000, Kuongeza mapato ya Serikali na kurasimisha kazi zao, ili kuwawezesha kupata mikopo ya Serikali kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa. Kanuni za Baraza Kifungu cha 20 (a)-(b) na (i), serikali kurasimisha kazi zao ili kuwawezesha kupata mikopo ya serikali kupitia mfuko wa utamaduni na sanaa. Hapa sanaa iko kwenye kupamba siyo kutengeneza keki.

Miundombinu ya saluni za kike na kiume watatozwa 10,000 Kuongeza mapato ya Serikali na kurasimisha kazi zao ili kuwawezesha kupata mikopo ya serikali kupitia mfuko wa utamaduni na sanaa

Wabunifu wa Mavazi (Fashion and textile designers) watalipa 10,000 ili kuongeza Kuongeza mapato ya Serikali na kurasimisha kaz zao Sheria Na. 23 ya 1984 Kifungu cha 2 (a) (i) – (vi) Kanuni za Baraza Kifungu cha 20 (b).

Related Articles

Back to top button