Wanasiasa wataka uchunguzi kuuzwa kwa Kampuni ya Warner Bro

NEW YORK: KATIKA hatua kubwa ya kihistoria, kampuni ya Warner Bros. Discovery inayojishughulisha na utengenezaji wa filamu, vipindi vya televisheni na maudhui ya kidigitali imekubali kununuliwa na Kampuni ya Paramount Skydance kwa takribani dola bilioni 110.
Dili hilo linaelezwa kuwa moja ya makubwa kuwahi kutokea katika tasnia ya burudani duniani.
Kinachovuta zaidi hisia ni kwamba Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, David Zaslav, anatarajiwa kunufaika kwa kiasi kinachokadiriwa kufikia dola milioni 667 kama fidia na malipo mbalimbali baada ya mauzo hayo kukamilika.
Malipo hayo yanajumuisha fedha taslimu, hisa pamoja na bonasi maalum, huku sehemu ya fedha hizo ikitegemea muda ambao mchakato wa ununuzi utakamilika.
Hata hivyo, dili hilo bado linakabiliwa na changamoto za kisheria nchini Marekani, ambapo baadhi ya wanasiasa wameomba uchunguzi kufanyika ili kubaini athari zake kwenye ushindani wa soko na usalama wa taifa.




