Africa

Wachezaji Yanga kuzawadiwa

RAIS wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amewaahidi wachezaji wa timu hiyo kuwa watapata zawadi ya fedha endapo wataifunga Al Hilal katika mchezo wa kwanza kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika Oktoba 8.

Akizungumza na Spotileo Hersi amesema mchezo huo ni mgumu na muhimu kushinda kwa kuwa Yanga ipo nyumbani hivyo uongozi umeamua kuwaongezea ari wachezaji ili kupata ushindi.

Hata hivyo Hersi amesema kwa sasa hawezi kusema ni kiasi gani cha fedha ambacho watawapa wachezaji endapo watashinda mchezo huo lakini kitakuwa kikubwa.

“Hivi ni vitu vya kawaida na siyo mara ya kwanza kuwapa motisha wachezaji wetu pindi tunapokwenda kwenye mchezo muhimu kama wa Jumamosi. Kwa maandalizi yetu na ubora wa kikosi chetu naamini hiyo itakuwa kama mitisha kwao,” amesema Hersi.

Amesema malengo ya Yanga ni kumaliza mchezo huo Dar es Salaam ili wawe na kazi ndogo watakapokwenda Sudan kwenye mchezo wa marudiano ambao ndio utatoa mshindi wa jumla.

Related Articles

Back to top button