EPL

“Wabaguzi hawaniyumbishi” – Tel

LONDON: MSHAMBULIAJI wa Tottenham Hotspurs, Mathys Tel amesema hataruhusu kuyumishwa na ubaguzi wa rangi unaoelekezwa kwake mtandaoni kufuatia kukosa penalty kwenye mchezo wa UEFA Super Cup dhidi PSG wiki iliyopita.

Katika chapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram Tel aliandika kuwa alivunjika moyo kwa tukio hilo lakini akasisitiza kuwa hatakata tamaa kupambania kipaji chake na kuipigania klabu yake

“Mimi pia nilivunjika moyo juu ya matukio yale lakini niseme tu kwamba matukio kama yale hayana nafasi kwetu kama familia ya soka na katika jamii yetu. Najua nilipotoka, nilipoanzia na hakuna hata moja ya haya kitakachoniangusha. Kwa kazi na unyenyekevu, heshima itatawala.” Tel ilichapisha kwenye mtandao wa kijamii Jumanne.

Mshambuliaji wa Bournemouth Antoine Semenyo pia alikutana na kadhia hii ya ubaguzi wa rangi wakati timu yake ilipochapwa 4-2 na Liverpool kwenye uwanja wa Anfield Ijumaa.

Tayari Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 47 kutoka jijini Liverpool amekamatwa kwa tuhuma za kumbagua Semenyo amepewa dhamana kwa masharti na kupigwa marufuku kuhudhuria mechi za soka.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button