Vodacom Cycling Tour yaenzi fikra za Nyerere


Waendesha baiskeli wakiingia nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwitongo, Butiama mkoani Mara, wakati wa kuhitimisha msafara wa Vodacom Nyerere Cycling Tour 2026, msafara huo umedhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc na kushirikisha zaidi ya waendesha baiskeli 200.

Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Madaraka Nyerere (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Vodacom Tanzania PLC na Stanbic Bank Tanzania wakati wa kilele cha msafara wa Baiskeli wa Vodacom Nyerere Cycling Tour 2026 zilizofikia tamati Butiama, mkoani Mara leo. Hafla hiyo ni sehemu ya Vodacom Nyerere Cycling Tour 2026, inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc, ili kuenzi fikra za Mwalimu Nyerere kupitia michezo na miradi ya maendeleo ya jamii.

Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Madaraka Nyerere (katikati), akizungumza na Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kushoto) na Mkurugenzi wa Tehama wa kampuni hiyo, Athumani Mlinga, wakati wa hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere iliyofanyika Mwitongo, Butiama mkoani Mara. Tukio hilo ni sehemu ya Vodacom Nyerere Cycling Tour 2026, inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc, ili kuenzi fikra za Mwalimu Nyerere kupitia michezo na miradi ya maendeleo ya jamii.

Waendesha baiskeli walioshiriki Nyerere Cycling Tour 2026 wakiwa nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwitongo, Butiama mkoani Mara, wakati wa kuhitimisha msafara huo uliohusisha zaidi ya waendesha baiskeli 200 na kufadhiliwa na Vodacom Tanzania.

Mkurugenzi wa Tehama wa Vodacom Tanzania Plc, Athumani Mlinga, akizungumza na washiriki wa Vodacom Nyerere Cycling Tour 2026 katika kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara, wakati wa kuhitimisha msafara huo ulioandaliwa kwa lengo la kuenzi fikra za Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Waendesha baiskeli walioshiriki Nyerere Cycling Tour 2026 wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc katika kijiji cha Mwitongo, Butiama, mkoani Mara, baada ya kuhitimisha msafara wa kilomita 1,450 kutoka Bagamoyo, uliofanyika kwa lengo la kuenzi urithi wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, huku ukihamasisha maendeleo ya jamii kupitia michezo.




