EPLKwingineko
Vigogo vitatu England vyamtupia macho Mamardashvili

KLABU za Ligi Kuu England za Manchester United, Chelsea na Tottenham Hotspur zina nia kumsajili golikipa wa kimataifa wa Gerogia anayekipiga Valencia, Giorgi Mamardashvili.
Ripoti zimesema wakala wa mchezaji huyo alikwenda London kujadili suala la uhamisho wake.
Magolikipa wa timu hizo tatu David de Gea, Edouard Mendy na Hugo Lloris wanarajiwa kuondoka timu hizo za EPL.
Hata hivyo kumhamisha Mamardashvili kutoka Valencia huenda kukawa kugumu kutokana na nyota huyo kusaini mkataba mpya Septemba, 2022.
Dili la uhamisho wake linaaminika kujumuisha kipengele cha kumwachilia chenye thamani ya pauni milioni 87.5 sawa na shilingi bilioni 253.9.