Nyumbani

Uzinduzi, viingilio Wiki ya Mwananchi hivi hapa

BAADA ya Yanga kutangaza kuwa kilele cha Wiki ya Mwananchi 2023 kutafanyika Julai 22, sasa imetangaza uzinduzi wa wiki hiyo.

Taarifa Yanga kupitia mitandao ya kijamii imesema wiki hiyo itazinduliwa Julai 15 mkoani Mwanza ikihusisha matukio mbalimbali ya kijamii na burudani.

Viingilio wakati wa killele hicho ni VVIP 500,000/-, Royal 300,000/-, VIP A 100,000/-, VIP B 40,000/-, VIP C-1 30,000/-, VIP C-2 20,000/- na mzunguko 10,000/-.

Yanga itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa  dhidi ya Kaizer Chiefs ya Africa Kusini kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wakati wa kilele hicho.

 

 

Related Articles

Back to top button