EPLKwingineko

United kuchukua hatua dhidi ya Ronaldo

KLABU ya Manchester United imesema inapanga kuchukua hatua zinazostahili baada ya mahojiano ya Cristiano Ronaldo ambapo alisema “klabu imemsaliti”

Mshambuliaji huyo wa kireno alisema hamheshimu kocha Erik Ten Hag kwa sababu kocha huyo hamheshimu yeye na analazimishwa kuondoka Old Trafford.

“Leo asubuhi Manchester United imeanza mpango wa kuchukua hatua zinazostahili kutokana na mahojiano ya hivi karibuni ya Cristiano Ronaldo na vyombo vya habari,” taarifa ya klabu hiyo imesema.

Taarifa imesema klabu haitatoa kauli nyingine zaidi hadi mpango huo umefikia tamati.

Baada ya mahojiano mapana na Piers Morgan kwenye televisheni ya Talk ya Uingereza, hatma ya Ronaldo ndani ya Man Utd iko mashakani.

Mkataba wa Ronaldo katika klabu ya Manchester United unamalizika Juni 30, 2023.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 ataiongoza Ureno katika michuano ya Kombe la Dunia Qatar 2022 mchezo wa kwanza wa nchi hiyo kundi H ukiwa dhidi Ghana Novemba 24 utakaofanyika uwanja wa 974 uliopo mji mkuu wa Qatar, Doha.

 

Related Articles

Back to top button