Europa

Ulinzi waimarishwa usiku wa Uefa

ULINZI mkali utaimarishwa kuelekea michezo ya Ligi ya Mabingwa kufuatia taarifa ya chombo kimoja cha habari kilichoripotiwa kuunga mkono kundi moja lenye itikadi za kidini  katika jiji la Madrid.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) limesema linafahamu kuhusu vitisho hivyo lakini michezo hiyo Arsenal na Bayern Munich, Dortmund na Atletico Madrid itaendelea kama ilivyopangwa.

Mawaziri wa Ufaransa na Uhispania wamethibitisha kuimarishwa kwa hatua za usalama.

BBC wameripoti kuwa kituo cha vyombo vya habari kinachounga mkono IS kimechapisha mabango mengi yanayotaka mashambulizi katika viwanja vitakavyotumika michezo hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button