CHAN

‘Tumejipanga vizuri CHAN2024’, Msitha

DAR ES SALAAM: Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha amesema, Tanzania imejipanga vizuri maandalizi ya kuelekea ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN2024), yanayotarajia kuanza Agosti 02, 2025, ambapo Tanzania itakuwa na mchezo wa ufunguzi dhidi ya Burkina Faso katika uwanja wa Benjamin Mkapa siku hiyo.

Msitha ameyasema hayo Leo Julai 25, 2025 alipokuwa kwenye mahojiano na Kituo cha Clouds TV katika kipindi cha ‘Power Breakfast’ ikiwa ni maandalizi ya kuelekea ufunguzi wa michuano hiyo.

“Hili ni shindano la Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika, kwa hiyo unapopata uenyeji kunakuwa na ‘conditions’ kwamba kwenye eneo la miundombinu ya viwanja wanataka iweje-kwa hili tumejipanga vizuri kuanza kwa michuano hiyo” amesema.

Amesema wamejipanga kwenye maeneo yote yanayohusu huduma wakati wote wa michuano hiyo ambapo pia amesema ipo haja kwa watanzania, kutumia fursa hiyo kufanya biashara hususan za utoaji wa huduma.

“Kuanzia hoteli, watendakazi, pia najisikia fahari kusema kwa kiasi kikubwa mambo yote ambayo walituelekeza kuyafanya, tumeyafanya na kuyakamilisha kwa ngazi ambazo wanazitaka wao” amesema Msitha

Related Articles

Back to top button