La Liga

Trent aiweka njiapanda Madrid

MADRID: Beki wa mabingwa wa kihistoria wa Ligi Ya Mabingwa Ulaya Real Madrid, Trent Alexander-Arnold amepata jeraha kwenye mguu wa kushoto siku chache kabla ya klabu yake kukutana na Manchester City.

Beki huyo wa kulia aliumia misuli ya juu ya mguu wa kushoto na akifanyiwa mabadiliko muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza katika ushindi wa mabao 3-0 wa Real Madrid dhidi ya Athletic Bilbao usiku wa Jumatano.

Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool tayari alishakosa takribani wiki sita mapema msimu huu kutokana na jeraha tofauti kwenye mguu huo huo wa kushoto. Alikuwa ameanza mechi nne mfululizo kwenye kikosi cha Xabi Alonso kabla ya kupata pigo hili jipya.

Real Madrid haikuweka wazi muda wa mapumziko utakaohitajika, lakini jeraha linaibua wasiwasi kutokana na ratiba iliyosongamana ya klabu hiyo. Madrid inakutana na Celta Vigo Jumapili kwenye La Liga kabla ya kuwakaribisha Manchester City siku tatu baadaye kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Madrid pia inakabiliwa na ukosefu wa wachezaji katika nafasi hiyo, baada ya beki mwingine wa kulia, Dani Carvajal, naye bado hayupo kwenye hali bora baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa goti.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button