EPL

Tottenham yahamia kwa Mbeumo

LONDON: Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Tottenham zinasema kuwa viongozi wa klabu hiyo sasa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Brentford Bryan Mbeumo baada ya ‘perfomance’ ya kuridhisha ya Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon aliyeingia kambani mara 20 katika Ligi Kuu msimu uliopita.

Hii inakuja baada ya Spurs kumsaini Meneja wa zamani wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka klabu ya Brentford, na uongozi unaamini kocha wao mpya Thomas Frank angependa kuwa na mshambuliaji huyo Spurs.

Kufikia mapema mwezi huu, Mbeumo alikuwa akihusishwa na Manchester United iliyoweka mezani Euro milioni 45 na bonasi ya Euro milioni 10. Hata hivyo hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati ya klabu hizo mbili huku ofa hiyo ya United ikikosa thamani wanayotaka Brentford

Vyanzo mbalimbali vya vya habari vimeiambia BBC Sport kwamba Spurs bado hawajawasilisha rasmi ofa ya kumnunua Mbeumo huku klabu zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu ujao vikipigana vikumbo kumnunua raia huyo wa Cameroon.

Imefahamika kuwa hakuna kipengele cha kutolewa (release clause) katika mkataba wa Mbeumo, ambao bado umebakiza mwaka mmoja kumalizika, ingawa kuna kipengele cha kuruhusu kuongeza mwaka mwingine.

Mbeumo amefunga mabao 70 katika mechi 242 akiwa na Brentford tangu alipowasili London Magharibi mwaka 2019 akitokea klabu ya Troyes ya Ligue 2 nchini Ufaransa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button