Europa

Tetesi za usajili Ulaya

KLABU ya Saudi Pro League Al-Ittihad iko tayari kutoa pauni milioni 70 kwa mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah msimu huu wa joto. (Talk sport)

Chelsea wanataka kupata ofa ya pauni milioni 43 kwa mshambuliaji wa Athletic Bilbao Nico Williams, 21, kabla ya dirisha la uhamisho kufunguliwa. (Football Insider)

Manchester City wamekubaliana na kiungo wa kati wa West Ham wa Brazil Lucas Paqueta mwenye umri wa miaka 26 kabla ya uhamisho wa majira ya joto. (Mercato France)

Liverpool wamempa meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim kandarasi ya miaka mitatu kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp. (Pedro Sepulveda kupitia GiveMeSport)

West Ham, Liverpool, Tottenham na AC Milan wanamtaka beki wa Fulham mwenye umri wa miaka 26 Tosin Adarabioyo, ambaye kandarasi yake inamalizika msimu wa joto. (Guardian)

Liverpool, Newcastle United na AC Milan wanafikiria kumnunua winga wa Leeds United Mholanzi Crysencio Summerville, 22. (Football transfer).

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button