Europa

Onana akubali lawama

MPAKA sasa kipa wa Manchester United, Andre Onana ameruhusu mabao 14 katika michezo sita msimu huu.

Kati ya mabao hayo, manne ameruhusu katika mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munchen ulioisha kwa United kupoteza mabao 4-3 Allianz Arena.

Stori kubwa katika mabao hayo ni namna alivyofungwa bao la kwanza lililofungwa na Leroy Sane ambapo baada ya mechi Onana amekubali makosa na kubeba lawama zote.

Ni wajibu wangu kwa sababu yangu ndio maana hatukushinda na lazima nijifunze kutokana na hilo, nina mengi ya kuthibitisha kwa sababu kusema ukweli mwanzo wangu Man United sio mzuri sana, ni mimi niliyeiangusha timu.” Amesema Onana.

Jumamosi katika mwendelezo wa EPL, United itacheza na Burnley, Jumanne Oktoba 3 itakuwa Old Trafford kuwakaribisha Galatasaray Ligi ya Mabingwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button