Ligi KuuNyumbani

Tanzania Prisons mambo magumu

TANZANIA Prisons mambo sio shwari kwa upande wao kwani takwimu za mechi tano
walizocheza zinaonesha hawajashinda mchezo hata mmoja.

Mpaka sasa wamecheza michezo 23 na kati ya hiyo wameshinda mitano, sare saba na kupoteza 11.

Katika michezo mitano iliyopita, imepata sare moja pekee lakini michezo minne hakuna ushindi wowote kuonesha ni hatari kwao kama wasipojitahidi michezo saba iliyobaki wanaweza kushuka daraja.

Mchezo wao uliopita walikuwa ugenini mjini Moshi ambako walipoteza dhidi ya Polisi Tanzania bao 1-0.

Akizungumza na gazeti la HabariLEO Kocha Msaidizi wa Prisons, Shaban Mtupa amesema ushindani umekuwa mkubwa kwani wamekuwa wakijipanga vizuri kwa lengo la kupata ushindi lakini wanajikuta wakipoteza.

“Tumekuwa tukifanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kushinda lakini na wenzetu wanajiandaa. Kila mchezo umekuwa na ushindani na mgumu lakini bado tunaendelea
kufanya marekebisho kujiweka imara,” amesema.

Amesema bado wana nafasi hajakata tamaa wataendelea kupigania pointi tatu kwa kila mchezo ulioko mbele yao kuhakikisha wanashinda na kujiondoa kwenye hatari ya kushuka
daraja.

Timu hiyo inashika nafasi ya 14 kwa pointi 22 ambazo hazitoshi kuwaaminisha nafasi yao ya kubaki Ligi Kuu.

Prisons imebakiza mechi ngumu saba ambazo ni dhidi ya Coastal Union, Namungo, Ruvu Shooting, Geita, Kagera Sugar, KMC na Yanga.

Timu pekee ambazo zinaweza kuwa salama kwa asilimia 99 ni zile zinazoshika nne bora za juu. Yanga, Simba, Singida Big Stars na Azam FC.

Related Articles

Back to top button