La Liga

TAA amwaga Kihispania akitambulishwa Madrid

MADRID, Beki wa kulia wa Uingereza Trent Alexander-Arnold ameelezea kujiunga kwake na Real Madrid kama “ndoto iliyotimia” na “jukumu kubwa” alipokuwa akihutubia mamia ya mashabiki walofika kushuhudia utambulisho wake hotuba aliyoitoa kwa lugha ya Kihispania.

Alexander-Arnold, mwenye miaka 26, angeweza kuondoka Liverpool kama mchezaji huru mkataba wake utakapokamilika tarehe 30 Juni lakini mabingwa mara 15 wa Ulaya Real waliwalipa Liverpool ada ya kumwachilia mapema ili aweze kuwachezea Los Blancos kwenye Kombe la Dunia la Klabu linaloanza kutimua vumbi wikiendi hii.

Video inayomuonesha Alexander-Arnold kama mchezaji mdogo pamoja na mabao yake, pasi za mabao (asist) na ile akitekeleza majukumu yake ya kiulinzi Liverpool na Uingereza ilichezwa kabla ya rais wa Real Florentino Perez kumkaribisha beki huyo wa kulia kwenye klabu hiyo.

Alexander-Arnold, ambaye aliketi na mpenzi wake, Estelle Behnke, wazazi wake Pamoja na ndugu zake wengine, alipanda jukwaani na kuhutubia mashabiki wa Real Madrid ambao ni pamoja na beki wa kushoto wa zamani wa Madrid Roberto Carlos kwa lugha ya Kihispania.

“Asante sana Rais Florentino Perez na Real Madrid kwa nafasi hii,” alisema.

“Kujiunga na klabu kama Real Madrid si jambo linalotokea kila siku. Ni ndoto iliyotimia. Nina furaha sana na ninajivunia kuwa hapa. Nina hamu ya kuionesha klabu na mashabiki kile ninachoweza kufanya.”

“Niko tayari kujitolea jasho na damu kwa ajili ya timu na mashabiki wa Real Madrid. Nataka kuwaonesha kile ninachoweza kufanya, nataka kushinda mataji mengi sana hapa, kuwa bingwa, na kuendelea kukua na kufurahia soka nikiwa na wachezaji bora zaidi duniani.” Alexander-Arnold alisema yuko

Bingwa huyo mara mbili wa Ligi kuu ya England baadae alipiga picha na rais Perez wakiwa wameshikilia jezi ya Real Madrid, yenye jina Trent badala ya Alexander-Arnold iliyoandikwa kwenye jezi ya Liverpool, na nambari 12 badala ya 66 aliyovaa Liverpool.

Related Articles

Back to top button